Rais Samia Kuwa wa Kwanza Afrika Kutwaa Tuzo ya The Gates Goalkeepers Award

Rais Samia Kuwa wa Kwanza Afrika Kutwaa Tuzo ya The Gates Goalkeepers Award

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” ikitambua mchango wake katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.

Tuzo hizi zilianza kutolewa mwaka 2017 na Taasisi iliyojulikana kama Bill and Melinda Gates Foundation (BMGF), kuanzia mwaka 2024 taasisi hii ilijulikana kwa jina la Gates Foundation (GF).

Tuzo hizi zilianzishwa ili kuwaleta viongozi wakubwa wa kisiasa ili kuchochea kasi ya kufikia Malengo Endelevu ya Kimataifa “Sustainable Development Goals, SDG”, ifikapo mwaka 2030.

Rais Samia Suluhu anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kupokea tuzo hiyo. Miongoni mwa viongozi waliowahi kupata tuzo hiyo ni Mheshimiwa Luiz Lula da Silva (Rais wa Brazil), Ursula Von der Leyen (Rais European Commissioner), Phumzile Mlambo Ngciuka (Makamu wa Rais, Afrika ya Kusini) na Narendra Modi (Waziri Mkuu wa India).

Kwa upande wa Tanzania Rais Samia Suluhu amefanikisha ongezeko la bajeti ya kuimarisha huduma ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kusogeza huduma za dharula za uzazi karibu na wananchi kwa kujenga zaidi ya vituo 530 vya upasuaji wa kutoa mtoto tumboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published.